Virusi vya corona: 'Wazazi hawana uwezo wa kuniwezesha kudurusu mtandaoni'

Maelezo ya video, Virusi vya corono: 'Wazazi hawana uwezo wa kuniwezesha kudurusu mtandaoni'
Iliyochapishwa

Covid -19 imefichua ukosefu wa usawa katika taasisi za elimu Kenya

Umasikini, ukosefu wa huduma za intaneti na ukosefu wa nguvu za umeme imewafanya baadhi ya wanafunzi kushindwa na kupata nafasi ya kuendelea na masomo wakati huu ambao shule zimefungwa.

Mitihani ya kitaifa nchini Kenya imepangiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu baada ya shule kufungwa Machi 2020, kutokana na janga la corona.

Video na Anne Okumu