Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wafanyakazi wahamiaji walalamikia kutupwa nje ya ubalozi wa Ethiopia mjini Beirut
Iliyochapishwa
Wafanyakazi wa ndani wametelekezwa nje ya ubalozi mjini Beirut, wakati kukiwa na mgogoro wa kiuchumi Lebanon, uliosababishwa na janga la corona. Uchumi wa Lebanon unaporomoka huku nchi hiyo ikipoteza 70% ya thamani ya sarafu yake katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Zaidi ya wafanyakazi wahamiaji 100 raia wa Ethiopia wametelekezwa nje ya ubalozi wao siku za hivi karibuni.