Mwafrika aliyelala mitaani Uingereza akiwa na ujauzito wa miezi saba.

Chanzo cha picha, Sarah Kamati
Sarah alilazimika kuchagua njia yenye changamoto : kuishi katika nchi alikozaliwa na kuendelea kubakwa na kuteswa au kukimbia na kuishi na msichana wake wa umri wa miaka 10.
Wakati huo akiwa na umri wa miaka 29-aliamua kutoroka nchi yake. Pale alipokua salama, alimleta binti yake.
Sarah, ambaye alikua na ujauzito wa miezi saba, aliwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Heathrow na mpenzi wake asubuhi tarehe 12 Disemba 2018. Lakini kile kilichoanza kama utaratibu mwepesi wa kuomba ukimbizi inadaiwa kiliishia kuwa kutoelewana ambako kuliwafanya wapenzi hao kukosa makazi ya kuishi.
Yafuatayo ni maelezo yake,akielezea maisha yake alipofika Uingereza.
'Tulikua na saa mbili za kuhama chumba'

Chanzo cha picha, Sarah
Tulipowasili katika Uwanja wa ndege wa Heathrow , tuliomba ukimbizi. Kila mtu alitusaidia sana, kutujali na kutuunga mkono.
Tulipelekwa katika hoteli ya Croydon ambako tulikaa vizuri. Tulihisi kuwa salama sana kuanzia chakula, na vipodozi tulipewa.
Lakini siku moja, baada baada ya kama wiki mbili, meneja wa hoteli alikuja chumbani kwetu na akasema kuwa alikuwa amepokea barua kutoka Wizara ya mambo ya ndani ikisema tulikua na "pesa zaidi ya za kutosha" kulipia gharama za kuishi, kwahiyo tulilazimika kuondoka.
Sikujua kama hilo lingetokea. Tulikua na pauni 600 tulizopewa tulipowasili, lakini wakati huo tulikua tumetumia kiasi kikubwa cha pesa hizo kwa matumizi ya chakula na nguo-kulikua na baridi sana-na tulinunua simu mpya.
Tulijaribu kumuelezea hali yetu, bila mafanikio. Maombi yetu ya ukimbizi yalikua yamekataliwa.

Chanzo cha picha, PA Media
Alitupa saa mbili tuwe tumeondoka katika chumba cha hoteli na akasema atatupeleka kwa gari atuache karibu na Lunar House-makao makuu ya Visa na uhamiaji ya Uingereza.
Ilikua inakaribia kabisa Christmas, kwahiyo hakuwa na uhakika kama kutakua na mtu yeyote wa kutusaidia katika ofisi ile, lakini kutupeleka huko ndio kitu pekee alichoweza kukifanya.
Nilihisi kama dunia nzima inapasuka. Hatukua na popote pa kwenda.
'Tulilala chini ya madaraja na vituo vya treni'

Chanzo cha picha, Sarah
Ofisi ya Lunar House ilikua imefungwa. Tuliketi chini kwenye benchi nje ya jengo bila kuamini yaliyotutokea. Tulikaa pale kwa saa kadhaa, bila kujua kabisa la kufanya. Tulishtuka sana.
Nilijifunika ndani kitambaa , lakini kulikua na baridi kali. Nilikuwa na wasiwasi ninaweza kumpoteza mtoto wangu aliyekua tumboni.
Saa chache baadae, mpitajnjia alituambia kulikua na daraja karibu. Lilikua umbali wa maili tatu ukitembea kwa miguu.
Tulitumia daraja hilo kama mahala pa kulala kwa siku kadhaa, tukatumia pesa yetu ya mwisho kwa chakula na vinywaji, na wakati mwingine tukilala kwenye vituo vya treni.
Sikuwahi kufikiria kwamba siku moja nitakuwa mtu ambaye hana makazi au kulala kwenye mitaa ya Uingereza. Sikujua mambo kama hayo yanaweza kutokea kwangu.
Nilikua nimekimbia Namibia kwasababu nilihofia maisha yangu. Nilitoroka kuepuka maisha ya kubakwa na kuteswa niliyoishi tangu nikiwa na umri wa miaka tisa.
Na sasa ninahofu ninaweza kufa katika baridi kali na barafu, ninawasiwasi kuwa ninaweza kumpoteza mtoto wangu na yote yangekua hayana maana.
'Nilikimbizwa hospitali'

Chanzo cha picha, Sarah
Baada ya siku 5 nikilala vibay, mkunga wangu - ambaye ningepewa anisaidie katika kipindi cha wiki mbili nchini -alinikutanisha na shirika la wasio na makazi la homeless charity Crisis.
Walitupa makazi ya muda kadhaa ya kulala hadi mapema mwezi Januari na wakatusaidia kuwasilisha tena maombi ya ukimbizi.
Halafu, siku moja, sikuweza kumsikia mtoto wangu akicheza tumboni, kwahiyo nilikimbizwa hospitalini.
Nilifanyiwa vipimo vya matibabu ambavyo vilionyesha kuwa mimi na mwananguo sote tuko salama, lakini wahudumu wa hospitali hawakuniruhusu kuondoka hadi walipohakikisha kuwa nina mahala salama pa kwenda.
Walitusaidia kufuatilia Wizara ya mambo ya ndani kuhusu maombi yetu ya uhamiaji, na katika siku ya tatu nikiwa hospitali, hatimae wizara ya mambo ya ndani iliidhinisha maombi yetu ya uhamiaji na ikatupeleka katika kituo cha afya chaThornton.
Kukataliwa kwa maombi yetu ya awali kulitokana na kosa katika maombi yetu ya uhamiaji.
Ilikua ni ahueni kubwa.
'Ninahisi kama nimemkosea binti yangu'

Chanzo cha picha, Handout
Nilijifungua Februari 2019 mwanangu wa kiume na mwezi Machi tuliwekwa katika nyumba moj mashariki mwa London.
Hatimae maisha yalisonga mbele tena.
Nilipata marafiki wachache, na nikaanza kwenda katika Magpie - ambalo ni shirika linalowasaidia akinamama na watoto wadogo wanaoishi katika mazingira yasiyo salama au makazi yasiyo salama-ambako niliweza kwenda na mtoto wangu mchanga, kupata nepi, kujumuika na wanawake wengine na kufanya shughuli nyingi.
Lakini ukaja mlipuko wa virusi vya corona, kila kitu kikasimamishwa.
Magpie waliniunganisha na shirika lingine la misaada linaloitwa Beam, ambalo kwa sasa linachangisha pesa kwa ajili ya kununua kiti cha juu na programyu za elimu kwa ajili ya mtoto wangu na laptop ili niweze kuboresha kiingereza changu na labda nipate kazi mara baada ya kuhakikishiwa uhalali wangu wa kuishi Uingereza.

Chanzo cha picha, Sarah
Laptop itakua ni nzuri kuipata wakati huu tunapojitenga.
Kutokana na kwamba sina la kufanya, ninajawa na wasiwasi kila siku, ninamhofia binti yangu Beverley.
Ninahisi ni kama nimemkosea, kwamba simlindi, kwamba nimekua mbinafsi.
Ninatamani suala langu lingetatuliwa haraka, kwasababu ni wakati huo tu ninaweza kudai kuungana na familia yangu ili bionti yamngu aweze kuungana nami.
Natamani angekua hapa na sisi, ili maisha yangu hatimae yaanze.
Wizara ya mambo ya ndani ilisema "imejitolea kuhakikisha kwamba madai ya uhamiaji yanchunguzwa kwa wakati unaofaa " na kwamba maamuzi yote yanachukuliwa "kwa misingi ya ushahidi uliopo wakati huo ".












