Bonde la Galwan: Picha zimeonyesha kwamba vyuma vilivyowekwa misumari ndio vilivyotumika katika vita kati ya India na China

Picha iliosambaa sana katika mitandao ya kijamii nchini India inaonesha vyuma vya misumari vilivyotumiwa na China katika vita vyake na India katika mpaka unaopiganiwa na mataifa hayo mawili.
Vita hivyo vilivyofanyika katika bonde la Galwan viliwaacha takriban wanajeshi 20 wa India wakiwa wamefariki na kuzua hofu kati ya mataifa hayo mawili.
China haikutangaza kuhusu kuwepo kwa majeruhi upande wake .
Pande zote mbili zilishutumiana kwa kuingia katika ardhi yake.
Mpaka kati ya mataifa hayo mawili umechorwa vibaya na unaweza kuhama kutokana na mabadiliko ya ardhi.
Picha iliojitokeza siku ya Alhamisi ilionyesha silaha butu ambazo zinadaiwa kutengenezwa na vyuma vilivyounganishwa na misumari.
BBC ilipatiwa picha hiyo na afisa mkuu wa jeshi wa India katika mpaka wa India na China ambao wanasema kwamba silaha hizo zilitumiwa na China.
Mchambuzi wa masuala ya Ulinzi Ajai Shukla, ambaye mara ya kwanza alituma picha hiyo kupitia ujumbe wa twitter, alielezea utumizi wa silaha hizo kama kitendo cha ukatili.
Ukosefu wa bunduki unarudisha kumbukumbu za makubaliano ya 1996 kati ya pande hizo mbili kwamba bunduki na vilipuzi visitumke katika eneo linalozozaniwa katika mpaka huo , ili kuzuia kusambaa kwa mgogoro.
Picha hiyo ilisambazwa sana katika twitter nchini India, hatua iliozua hisia kali kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Hakuna afisa wa India au China aliyetoa tamko lake kuhusu picha hiyo.
Ripoti za vyombo vya habari zinasema kwamba wanajeshi walikabiliana katika mlima mmoja ulio na urefu wa mita 4,267 huku baadhi ya wanajeshi wakianguka katika mto Galwan ulio na maji baridi sana.
Vifo vya kwanza baada ya miongo minne
Pande hizo mbili zimekabiliana katika mpaka katika wiki za hivi karibuni, lakini makabiliano ya siku ya Jumatatu ni ya kwanza kusababisha vifo katika kipindi cha miaka 45.
Ripoti ambazo hazikuthibitishwa katika vyombo vya habari nchini India zimesema kwamba takriban wanajeshi 40 walifariki , lakini China bado haijatoa habari yoyote kuhusu majeruhi .
Baadhi ya wanajeshi wa India wanadaiwa kutoweka.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje nchini China bwana Zhao Lijian alisema India imevuka mipaka mara mbili kuishambulia na kuchokoza raia wa China., na hivyo kupelekea kuwepo kwa ghasia za kijeshi katika mipaka ya pande zote mbili", chombo cha habari cha AFP kimeripoti .
Siku ya Jumatano, China ilidai kuwa na mamlaka ya mji wa Galwan" - madai ya uongo yaliopingwa na India kwa kuchochea mambo ambayo si halisia".

Chanzo cha picha, EPA
Wananchi wa pande zote mbili wamekuwa wakiandamana dhidi ya ghasia zilizojitokeza katika mpaka wa Himalaya, wakati maafisa wamezungumzia jambo hilo kidemokrasia i ili kufikia muafaka.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje India, Anurag Srivastava alisema mawaziri wote wawili wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu siku ya Jumatano, na kukukubaliana kutatua tatizo lote kwa umakini zaidi".
"Kutoa madai ambayo hayapo na kukuza mambo kutasababisha kushindwa kuafikia maafikiano," bwana Srivastava alinukuliwa akisema katika mkutano na chombo kimoja cha habari nchini India.
Serikali ya India imetoa tamko baada ya Subrahmanyam Jaishankar kufanya mazungumzo na Wang Yi wa China ambaye alisema jeshi lilitaka kuharibu maeneo ya upande wa India katika mpaka wanaoumiliki.
Taarifa iliyotolewa imeishutumu China kusababisha ghasia kwa kupanga hatua ambazo wanawajibika moja kwa moja kwa vurugu na kuwataka China kuchukua hatua sahihi kusahihisha makosa yao. "
Kwa sasa,taarifa ya China inamnukuu bwana Wang akisema: "China inapinga tena na inataka India kufanya uchunguzi .. na kuacha uchochezi wote ili kuhakikisha kuwa jambo kama hili halijirudii tena"


Kwa nini hakukua na bunduki
Bonde la mto Galwan lililopo Ladakh, likiwa na hali mbaya ya hewa , liko upande wa kaskazini wa LAC na karibu na Aksai eneo linalozozaniwa lakini linadaiwa na India licha ya kutawaliwa na China
Hii sio mara ya kwanza kwa mataifa hayo majirani yenye silaha za kinyuklia kupambana bila silaha katika mpaka wao. India na China wana historia ya kuchukua kuingia katika himnaya jirani na kukabiliana katika mpaka huo wenye urefu wa km 3,440 (maili 2,100) yalipo katika mstari wa LAC
Mara ya mwisho pande hizo kupigana kwa silaha ilikuwa mwaka 1975 wakati askari wanne wa India waliuwawa katika pembezoni mwa kaskazini mashariki mwa jimbo la Arunachal Pradesh. Vurugu hizo zilitajwa na mwanadiplomasia wa zamani kuwa uvamizi wa bahati mbaya. Lakina hakuna risasi hata moja iliyofyatuliwa tangu wakati huo.
Chanzo cha makubaliano ya mwaka 1996 yanasema "taifa lolote haliruhusiwi kushambulia lingine kwa silaha aina yeyote ya moto... au hata kuwinda kwa silaha katika eneo la mpaka".
Lakini kumekuwa na migogoro ya aina nyingi kwa wiki za hivi karibuni katika mpaka huo. Mwezi Mei, wanajeshi wa India na China walipambana katika mpaka wa eneo la ziwa la Pangong, pia katika eneo la Ladakh, na kaskazini mashariki mwa jimbo la Indiala la Sikkim ambalo ni maili mia moja katika upande wa mashariki.
India imeishutumu China kwa kutuma maelfu ya wanajeshi katika bonde la Ladakh la Galwan na kusema China imechukua km 38,000 (14,700 sq miles) za eneo lao.
Mazungumzo kadhaa yalifanyika kwa miongo mitatu iliyopita bila kufikia muafaka wa mgogoro huo wa mpakani.












