Virusi vya corona: Daktari anayewasaidia wanawake wajawazito kukabiliana na athari
Iliyochapishwa
Wakati serikali ya Kenya ilipotangaza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku, ilimaanisha kuwa wanawake wengi wajawazito wanaohitaji usaidizi wa dharura wa kimatibabu muda wa amri hiyo walikua katika hatari kutokana na ukosefu wa usafiri.
Dkt Jemimah Kariuki daktari bingwa wa wanawake katika hospitali kubwa zaidi ya umma ya rufaa Kenyatta National Hospital alitoa nambari yake ya simu katika mitandao ya kijamii kwa ajili ya wanawake wajawazito wakati watu ‘walipokua wakisubiri serikali’ iweke ichukue hatua.
Aliweza kuwasaidia wanawake karibu kumi kujifungua kabla serikali iingilie kati na kutokana na mfano wake serikali iliweka nambari maalum ya simu ya kitaifa inayoweza kupokelewa mara moja na mpigaji kuhudumiwa.