Je ni ipi hatma ya Warundi waliolazimika kwenda uhamishoni kipindi cha Rais Pierre Nkurunziza?
Nini hatma ya Warundi wanaoishi uhamishoni baada ya kifo cha Rais Pierre Nkurunziza?
Marina Barampama alikuwa makamu wa pili wa rais wakati wa utawala wa Rais Pierre Nkurunziza.
Marina Barampama aliondolewa kwa kuonekana kumuunga mkono aliyekuwa wakati huo mwenyekiti wa chama tawala CNDD FDD Hussein Rajabu ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Burundi na kuchukuliwa kama kitisho kwa utawala wa Rais Nkurunziza.
Nkurunziza alidai Bi. Marina alikuwa akimhujumu na hakuwa anawajibika ipasavyo katika wadhifa wake wa makamu wa rais hivyo kumfuta kazi mwaka 2007.
Alikihama chama tawala na kujiunga na chama cha UPD na mwaka 2015 na kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho.
Baadaye alikimbilia uhamishoni akihofia maisha yake chini ya utawala wa Rais Nkurunziza. Sikiliza mahojiano yake na mwanahabari wa BBC Caro Robi akizungumzia vile alivyopokea kifo cha aliyekuwa mshirika wake na baadae hasimu?