Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
George Floyd: Mwandishi aelezea kwa nini ilikuwa vigumu kwa yeye kutazama video ya mauaji.
Tangu kanda ya video iliokuwa ikimuonesha afisa wa polisi mzungu akimwekea goti lake George Floyd katika shingo yake kusambaa , imekuwa vigumu kuipuuza.
Lakini mimi ni mwananamke mweusi , nilifanya uamuzi kwamba wakati huu sitatazama hiyo video. Kiakili na kimaumbile inakera kwa mimi kuitazama wakati ambapo mtu mwingine mweusi anauawa katika mikono ya polisi mzungu.
Najua kutakuwa na watu wengi watakaoniambia napaswa kufurahia video hiyo ikisambaa sana kote duniani kwasababu ilitoa ukweli - tatizo kubwa la kijamii ambalo limekuwa likiendelea kwa karne kadhaa nchini Marekani.
Kama mwandishi ni nini haswa kingekuwa bora kwangu zaidi ya kupata ukweli?
lakini miaka kadhaa sasa nimegundua kwamba kuna tofauti ndogo kati ya kufichua vitendo vya kutisha kama hivi na kulinda afya yangu ya kiakili, hususan wakati habari hiyo inaelezea niliyoyapitia.
Nadhani kila mtu anayeitazama kanda hii ya video itamuathiri kiakili, ukweli ni kwamba inaweza kuchochea matatizo ya kiakili.
'imepita kiasi'
Nilipozungumza na Nia Dumas , mwanamke mweusi anayeishi Marekani, aliniambia hawezi kujizuia kulia baada ya kutazama muda wa mwisho wa George Floyd.
''Nimejipata nikiwa ninalia, mara nyengine mara nne kwa siku tangu nilipoitazama'', alisema, Ni video inayotisha kwa kweli.
Nia anaishi Cleveland jimbo la Ohio, ambapo ameshuhudia ghasia nyingi.
Picha za watu weusi wakiuawa liilikuwa jambo la kawaida katika maisha.
''Iwapo sio George Floyd basi alikuwa mtu mwengine. Ilikuwa inakera kwa kweli'', alisema.
Kwangu mimi , kuona kanda hiyo ya mauaji kulichochea fikra za mauaji ya Trayvon Martin.
Nilikuwa na umri wa miaka 11 na inasikitisha kuona vitu kama hivyo kwa miaka kadhaa sasa. Nimechoka.
Trayvon Martin alikuwa kijana mweusi mwenye umri wa miaka 17 , ambaye alipigwa risasi na askari aliyekuwa jirani yao katika jimbo la Florida, ambaye hakupatikana na makosa yoyote kwa kuwa alikuwa akijilinda.
Yalikuwa mauaji ya Trayvon ambayo yalisababaisha kutumika kwa alama ya reli ya BlackLivesMatter.
'Nilivunjika moyo'
Tangu wakati huo, neno hilo limetumika mara kadhaa , kama alivyoniambia Toni Adepegba , Muingereza mweusi wakati tulipozungumza kuhusu ubaguzi na athari zake katika afya ya ubongo.
''Umekuwa mwezi mzito'', alisema.
Wiki moja tangu kusambaa kwa kanda ya video ya Ahmaud Arbery.
Nilikuwa sijapona tangu nilipoona kanda hiyo ya mauaji ya Ahmaud na nikaona imetokea tena.
Ahmaud Arbery mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akifanya mazoezi wakati alipopigwa risasi na kufariki wakati wa mgogoro na baba na mtoto wake katika jimbo la Georgia Marekani.
Mtangazaji wa redio wa BBC anaelezea uchungu wa video ya floyd.
Kwa Toni , kutazama kanda ya mauaji ya Floyd ilikuwa hali ngumu sana.
''Sina maneno ya kuelezea hisia hiyo. Nilihisi nimevunjika moyo. Nilihisi kuchoka kwaszbabu watu hawa wangekuwa mimi''.
Mapema siku hiyo hiyo, alitazama kanda ya nyengine ya video ya mwanamke mzungu wa mjini New York ambaye alikuwa akitaka usaidizi baada ya mtu mwengine mweusi kumtaka amfunge mbwa wake kulingana na sheria za bustani hiyo ya central Park.
''Ni kitu kilichokuwa kinakera'' , alisema Toni.
Kwasababu kilionesha wazi tofauti iliokuwepo , mwanamke huyo mzungu alikuwa anajua fursa aliokuwa nayo kama mwanamke mweupe dhidi ya mwanamume mweusi.
Alijua kwamba ana uwezo wa kumfanya mwanamume huyo akamatwe ama hata kuuawa kwa kutumia simu moja tu."
Toni alishindwa kuitazama kanda yote ya mauaji ya George Floyd.
fikira yangu ya kwanza nilipoiona , ni kwanini watu wamesimama tu hapo? lakini nadhani ni kwasababu walijua kwamba wangewekwa katika changamoto kama hiyo iwapo wangejaribu kuingilia kati.
Katika wiki za hivi karibuni , nimejadiliana na watu wengi iwapo kuna faida yoyote ya kuweka kanda hizi katika mitandao.
Laetitia Kandolo ni mwanamke mweusi mwenye umri wa miaka 28 ambaye familia yake inatoka DR Congo. Alishindwa kumaliza kuitazama kanda ya mauaji ya George Floyd.
Huu ndio ukweli uliopo
"Kulikuwa na hisia chungu nzima kuweza kuelezea. lakini saa chache baadaye wakati kanda hiyo ilipokuwa ikisambaa kwa haraka nilirudi kuitazama . Alikuwa ameshindwa nguvu na alitambuliwa kwa hali hiyo.
Laëtitia Kandolo, a creative director, works between France and the DRC
''Lazima tutafute njia za kuwawajibisha watu wabaguzi'' , anasema Laetitia.
Iwapo kanda hizi za video zitawalazimu wale walio katika nafasi kwasababu ya rangi ya ngozi yao kuwacha ubaguzi na kufikiria, basi ni vyema ziendelee kuwekwa katika mitandao.
Ni muhimu kukumbuka kwamba watu weupe wanatazama video hii, wakati ambapo sisi tunaiacha- huu ndio ukweli wetu.
Nia, kutoka Marekani, ana wasiwasi kuhusu uungwaji mkono anaouona mitandaoni, iwapo masuala muhimu kama vile fursa za wazungu na ubaguzi hayataangaziwa.
''Nataka kuona unachohisi, mafikra yako ama kile unachochangia katika mjadala, tumelifanya liwe jambo la kawaida kwa mtu kusambaza chapisho, kanda ya video kujibu ujumbe wa Tweet kwamba ni kuunga mkono....nadhani hilo limepita''.
Wakati watu weusi wanapopitia kanda hiyo wanajiona nyuma ya alama ya reli.
''Nilikuwa nikifanya mazoezi ya kukimbia usiku wakati kanda ya video ya Ahmaud ilipotokea'', alisema Toni.
Ilinijia kwamba huenda kuna watu wameniona nikikimbia na kuwapigia polisi simu kwa madai kwamba huenda nakimbia uhalifu niliotekeleza.
Na inanijia akilini mwangu kwamba iwapo ningekuwa raia wa Maarekani pengine ningekuwa yeye.