Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Mapadre wanaoamini corona ni 'kazi ya shetani'
Wakitembea mkono mmoja ukiwa umebeba msalaba na mwingine kitakasamikono, kikundi cha mapadre wa kikatoliki katika eneo la Metro Manila wamekua wakihatarisha maisha yao kuendelea. kuwahudumia watu wa jamii zilizokumbwa na umaskini.
Mji wa Manila umekuwa chini ya amri ya kutotoka nje inayotekelezwa na polisi na kwa miezi, lakini mamia ya watu wamekuwa wakipata maambukizi kila siku na upimaji wa virusi bado ni wa kiwango cha chini.
Howard Johnson na Virma Simonette waliwafuata makasisi ambao, huvaa mavazi kamili ya kinga ya maambukizi ya virusi vya corona (PPE), na kuendelea kutoa huduma ya kiroho kwa waumini wao.