Virusi vya corona: Viongozi wa dini waomba kufunguliwa kwa sehemu za kuabudu Uganda huku wagonjwa wakifikia 417

Maelezo ya sauti, Virusi vya corona: Viongozi wa dini waomba kufunguliwa kwa sehemu za kuabudu Uganda
Iliyochapishwa

Viongozi wa kidini nchini Uganda wametoa wito kwa serikali kuruhusu sehemu za kuabudu ikiwemo makanisa na misikiti kufunguliwa.

Sehemu hizo zilifungwa mwezi Machi katika juhudi za kupambana dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Wana mtazamo kwamba ikiwa usafiri wa umma utaruhusiwa kuanza tena wiki hii, basi hakuna sababu waumini wasijumuike kuabudu kama ilivyokuwa hapo awali.

Wito huu unakuja wakati wizara ya afya ikifichua kuwa wafanyakazi wake saba wamegunduliwa kuambukizwa virusi vya Corona.

Issaac Mumena ana taarifa ifuatayo.