Virusi vya corona: Korea Kusini yafunga shule tena baada ya maambukizi kuongezeka zaidi

Maelezo ya video, Mwanishi wa BBC Laura Bicker alitembelea shule moja kabla ya hatua ya kufungwa tena
Iliyochapishwa

Zaidi ya shule 200 nichini Korea Kusini zimelazimika kufunga tena shule siku chache baada ya kufunguliwa, kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Mapema Jumatano, melfu ya wanafunzi walirejea shuleni baada ya kufunguliwa tena nchini humo na kulegeza masharti yaliyowekwa awali kukabiliana na virusi vya corona .

Lakini baada ya siku moja tu, maambukizi mapya 79 yalirekodiwa, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kwa siku nchini humo kwa kipindi cha miezi 12.

Maambukizi haya mapya yalihusisha watu wa kituo kimoja ambacho kipo nje ya mji wa Seoul.

Ghala ambalo lililopo mji wa Bucheon, linaloendeshwa na kampuni kubwa ya kibiashara ya Coupang, na maafisa wanasema sehemu hiyo ilikuwa haitekelezi kikamilifu hatua za kuzuia maambukizi.

Maafisa wa afya walibaini maambukizi ya virusi vya corona katika viatu na mavazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

An empty classroom is seen ahead of school re-opening at Yeouido girl's high school on May 19, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Shule nchini Korea Kusini zimefungwa tena baada ya kurekodiwa kwa maambikizi zaidi kwa siku moja

Inawezekana Korea Kusini ikaendelea kurekodi maambukizi mapya wakati huu inapoendelea kupima maelfu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Maambukizi mapya 58 yalirikodiwa siku ya Ijumaa, na kusababisha taifa hilo kuwa na jumla ya idadi ya watu wenye maambukizi ya corona 11,402.

'Kitovu cha maambukizi'

Jumla ya shule 251 huko Bucheon zimelazimika kufungwa .

Imeripotiwa katika gazeti la Korea Times, kuwa Wizara ya Elimu imesema jumla ya shule 117 katika mji mkuu wa Seoul pia zimeahirisha tarehe ya kufunguliwa tena kwa shule.

Mwanafunzi mmoja mjini Seoul ambaye mama yake alikuwa akifanyakazi katika ghala la kampuni ya Coupang pia naye amepatikana na na virusi vya corona.

Pia unaweza kusoma:

Coronavirus

Sehemu za umma na maeneo ya historia katika mji wa Seoul zimefungwa, biashara pia zimefungwa na watu wametakiwa kutafuta namna nyingine ya kufanya kazi na kuzuia mkusanyiko wa watu wengi.

Korea Kusini ni miongoni mwa mataifa ambayo yalikumbana na athari kubwa ya mlipuko wa corona mwanzoni mwa mwaka huu lakini ikaonekana kuwa imeweza kudhibiti janga hilo kupitia mpango wa kutafuta, kupima kutibu watu.

Wiki za hivi karibuni, kumeonekana kuwa na maambukizi mapya kutokea, ikiwemo tukio moja lililohusisha mwanaume mmoja ambaye alitembelea vilabu vitano vya usiku mjini Seoul mji wa Itaewon mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Yonhap, maambukizi mapya 266 yamefuatiliwa kwa karibu huko Itaewon.

Unachohitajika kufanya ili kuzia mambukizi ya virusi hivi

Wataalam wa afya ya umma wamekuwa wakitoa ushauri ili kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi hivi.

Je nitajilinda vipi?

jinsi ya kulinda dhidi ya virusi
Presentational white space
Presentational white space
Tumia kitambaa kuziba
Iwapo huna tishu tumia sehemu yako ya mkono
Jizuie kugusa macho yako , pua na mdomo iwapo hujaosha mikono
Jiepushe na watu ambao ni wagonjwa
Presentational white space

Je dalili ni zipi?

Presentational white space
Hizi ndizo ishara za ugonjwa huu
Presentational white space

Nifanyeje iwapo sijisikii vyema?

Piga simu ili upate usaidizi
Presentational white space
Pia unaweza kushauriwa usalie nyumbani
Presentational white space
Unaweza kufanyiwa vipimo vya virusi
Presentational white space
Presentational grey line