Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Msichana aliyeendesha baiskeli ili kunusuru maisha ya baba yake amekuwa maarufu India
Msichana aliyeendesha baiskeli ili kunusuru maisha ya baba yake.
Jyoti Kumari, 15, amekuwa mashuhuri nchini India baada ya kuendesha baiskeli kwa kilomita elfu kadhaa akiwa amembeba baba yake aliyekuwa amejeruhiwa hadi kijijini kwao wakati wa janga la virusi vya corona.
Wawili hao walikuwa wamekwama mjini Delhi bila kuwa na namna yoyote ya usafiri wakati nchi hiyo ilikuwa inatekeleza amri ya kutotoka nje kama hatua ya kukabiliana na janga la virusi vya corona.
Hivi karibuni India ilianzisha tena usafiri wa njia ya treni na kusaidia wafanyakazi waliokuwa wamekwamba lakini ni idadi ndogo tu yao ambao hadi sasa wamefanikiwa kusafiri.