Virusi vya corona: Mama aliyekuwa na maambukizi ya Covid-19 ajifungua salama
Iliyochapishwa
Bi Silvia Kimaro alikuwa mjamzito aliyekuwa karibu kujifungua, wakati huo ndipo alipogundulika kuwa na ugonjwa wa Covid 19.
Hali hiyo ilibainika baada ya mumewe kumkimbiza hospitali ya Aga Khan akiwa na maumivu ya kifua. Alifanyiwa upasuaji na kupewa matibabu na kama anavyosimulia bi Silvia na mumewe Deogratias, ni muujiza kuwa mama na mtoto walitoka hospitali wakiwa salama na wenye afya.