Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya Corona: Fahamu namna ya kusali sala ya Idi nyumbani
Bila shaka mwezi mtukufu wa Ramadhan unaelekea kufika mwisho. Lakini wakati huu mambo ni tofauti kwasababu ya janga la virusi vya corona. Hivyo basi, nchi mbalimbali zimechukua hatua ili kuhakikisha virusi hivyo vinadhibitiwa miongoni mwayo ikiwa ni kutokaribiana, kunawa mikono mara kwa mara na kadhalika.
Lakini pia kwa wengi swala ya sikukuu ya Eid al-Fitr haitakuwa kama kawaida. Mfano nchini Kenya ni wazi kwamba waumini wa dini ya Kiislamu wanahitajika kusali sala hii nyumbani. Sasa je sala ya Eid al-Fitr inaswaliwa vipi nyumbani? Fuatilia maelezo ya Sheikh Hassan Kinyua.