Video inayomuonesha mwanahabari akimpatia viatu vyake mhamiaji yapata umaarufu mtandaoni

Iliyochapishwa

Maelfu ya wahamiaji nichini India wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kwa miguu kutoka mijini kurejea vijijini kwao. Wanahofia watakabiliwa na njaa wakisalia katika maeneo ya miji yaliyowekwa amri ya kutotoka nje, hatua ambayo imechukuliwa na serikali kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Mwandisi wa BBC Salman Ravi alikutana na mwanamume aliyekuwa ametembea umbali wa kilomita 250 bila viatu. Aliguswa sana na hali ya mtu huyo hadi akaamua kumpatia viatu vyake. Video hiyo imekuwa ikisambaa kwa kasi mtandaoni, huku baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wakisifia hatua ya mwanahabari.