Virusi vya corona: Je kwanini Waafrika wanaombwa kushiriki majaribio ya chanjo?

A generic photo of a masked nurse holding up a vaccine

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Na Anne Mawathe
    • Nafasi, Mhariri wa Masuala ya Afya, BBC Afrika
  • Iliyochapishwa

Kumekuwa na taarifa kadhaa za kuogofya kuhusu majaribio ya chanjo ya corona inayofanyiwa watu barani Afrika.

Hatahivyo, wanasayansi wanasema ni muhimu Waafrika washirikishwe katika majaribio ya chanjo, na kuongeza kuwa wasipofanya hivyo watalemaza juhuzi za kupatikana kwa chanjo itakayofanya kazi kote ulimwenguni- na wala sio kwa nchi tajiri pekee.

Mnamo mwezi Machi, Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus, alitangaza mkakati wa kimataifa wa "majaribio ya pamoja ya chanjo" kwa lengo la kutafuta dawa ya kutibu Covid-19, ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.

Kufikia sasa hakuna tiba iliyopatikana, na WHO linasema chanjo itasaidia kuzuia na kudhibiti na janga la corona.

Pia itasaidia mfumo wa kinga ya watu mwilini, kupigana na virusi na kuwazuia kuwa wagonjwa.

Jinsi Chanjo inavyofanya kazi:

  • Zinasaidia kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradi
  • Hii inasaidia kinga ya mwili kuzitambua na kubuni njia ya kukabiliana na magonjwa
  • Endapo mwili utaambukizwa maradhi ya kweli, utakuwa tayari kukabibiliana ikwani unajua lipi la kufanya
  • Chanjo kwa kawaida huchukua miaka kadhaa, kama sio miongo, kutengeza.
  • Chanjo ya Covid-19 itawezesha amri ya kutotoka nje kuondolewa na kulegezwa kwa hali ya watu kukaribiana
Chanjo ya corona

Kufikia sasa majaribio ya chanjo yameanza kufanya nchini Afrika Kusini - na moja inasubiri kuidhinishwa nchini Kenya.

Lakini suala hilo limekumbwa na mgogoro.

Mjadala wa sasa kuhusu majaribio ya chanjo, barani Afrika umejikita katika suala la ubaguzi wa rangi.

'dhana ya kikoloni'

Mjadala uliibuliwa na madktari wawili wa Ufaransa, waliokuwa wakijadiliana kuhusu majaribio ya chanjo barani Ulaya na Australia wakitathmini ikiwa chanjo ya kifua kikuu inaweza kukabiliana na virusi vya corona.

Katika mjadala huo uliokuwa ukioneshwa kwenye televisheni, wawili hao walikubaliana chanjo ifanyiwa majaribio pia Afrika , mmoja akasema: "Nauliza swali kizushi, kwanini tusifanye utafiti huu Afrika, ambako hakuna barakoa, wala matibabu maalum?.

Tamko hilo liliibua mjadala mkali uliolenga mtazamo wa mataifa ya magharibi dhidi ya Afrika.

"lilikuwa tamko la aibu na la kushangaza, katika karne 21, kutoka kwa wanasayansi," alisema Dkt Tedros,ambaye ni raia wa Ethiopia.

"Tuna laani tamko hilo kwa kinywa kipana, na tunawahakikishia kwamba hilo halitawahi kufanyika. Dhana hizo za kikoloni zilizopitwa na wakati lazima zikomeshwe."

Baadhi ya watu maarufu barani Afrika walilalamikia hatua hiyo, miongoni mwao wanasoka Didier Drogba na Samuel Eto'o - ambao wote ni waathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakiwa uwanjani walipokuwa wakicheza soka ya kulipwa barani Ulaya.

"Msiwachukulie Waafrika kama nguruwe! Inaudhi sana," Drogba aliandika kwenye Twitter yake.

Didier Drogba in 2018
AFP
Do not take African people as human guinea pigs! It's absolutely disgusting"
Didier Drogba
Ivorian ex-footballer

Ghadhabu kama hizo zina msingi kwasababu suala la ubaguzi kwa misingi ya rangi ya mwili na kiuchumi linasadikiwa kuwepo hususan katika sekta ya afya duniani.

Kuna ushahidi kuwa makampuni ya kutengeneza dawa zinafanya majaribio ya dawa zao katika baadhi ya sehemu Afrika, bila kujali maadili ama kuheshimu maisha ya binadamu.

"Kuna uwajibikaji na ulinzi mkubwa katika ngazi ya kibinafsi," Dkt. Kyobutungi, Mkuu wa kitengo cha utafiti wa watu barani Afrika (APHRC), aliiambia BBC.

"Ikiwa were ni mwanasayansi unayeshiriki katika utengenezaji wa chanjo, bila shaka hungelitaka kuona chanjo hiyo [ikiua] watu miaka michache baadae.

"Kwa hiyo wataalamu wanakuwa makini sana, kwani wamewekeza mengi katika taaluma zao."

Anasema pia kuna asasi za kitaifa zinazosimamia na kudhibiti masuala ya chanjo- ikama vile Baraza la kitaifa la sayansi na teknolojia Uganda(UNCST).

"Huwezi kufanya majaribio ya chanjo bila kuidhinishwa na assay kama hiyo ili kuhakukusha viwango vyote vya usalama vinazingatiwa.

Coronavirus
Banner

Richard Mihigo,ambaye anasimamia masuala chanjo na utengenezaji wake Katina shirk la WHO barani Afrika, anaungna mkono hilo.

"Katika mifumo yetu tunalinda na kutoa msaada wa kifedha ambao unawakinga Waafrika dhidi ya bidhaa zisizosalama."

Wale ambao wanfanya utafiti hawaruhusiwi kushiriki katika uuzaji wala utengenezaji wa dawa nyingine wala chanjo, aliongeza.

Hakikisho kama hilo mara nyingi hugubikwa na taarifa ghushi katika mitandao ya kijamiii zinazodai kuna njama ya kufanya majaribio ya chanjo hatari dhidi ya watu weusi kwa lengo la kuwaanganiza.

Maelezo ya video, Virusi vya Corona: Kwa nini ni muhimu kupima?

Kwa mfano, taarifa ghushi kuhusu vifo vya watoto saba nchini Senegal vilivyotokea baadaya kupewa kile kinachodaiwa kuwa majaribio ya chanjo ya Covid-19 ilizua ghadhabu katika mtando wa kijamii wa Facebook.

Taarifa hiyo lianza kusambazwa mitandaoni mapema mwezi Aprili baada ya kauli tata ya madaktari wa Ufaransa - ambayo ilipatia nguvu zaidi taarifa hiyo feki.

Maelezo ya video, Ni lini Chanjo ya corona itapatikana?

Malipo ya fidia

Jaribio tata la dawa lilifanywa na kampuin ya Pfizer katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria mwaka 1996.

Mgogoro wa kisheria wa muda mrefu wa uliibuka na hatimaye kampuni hiyo kubwa ya kutengeneza dawa ikalazimika kuwalipa fidia wazazi ambao watoto wao walishirikishwa katika majaribio ya dawa wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa utindio wa ubongo.

Watoto 11 walifariki na makumi ya wangine kupooza baada ya kupewa dawa ya kuzuia maumivu iliyokuwa ikifanyiwa majaribio.

Hatua hiyo ilizua swali la ikiwa wazazi wa watoto hao waliombwa idhini kabla na kama ya zoezi hilo liliendeshwa kwa uwazi.

Zaidi ya miongo miili baadaye, wanasayansi kama Catherine Kyobutungi kutoka Uganda wanasema mambo yamebadilika na mchakato huo unajumuisha hatua kadhaa na unafnywa kwa uwazi.

WHO limetaja usambazaji wa taarifa ghushi kama hali ''hatari" ambayo inastahili kupewa umuhimu.

Miongo kadhaa ya ufadhili mdogo

Lakini kale ambacho hakijapewa umuhimu ni kwa miaka kadhaa ni mifumo ya afya barani Afrika.

Licha ya ahadi ya mwaka 2001 iliyotolewa na viongozi wa nchi za Kiafrika ya kutenga angalau asilimia 15 ya bajeti Yao ya kila mwaka kuboresha sekta zao za afya bado ahadi hiyo haijatimizwa.

Taasisi ya Pasteur nchini Senegal inafanya utafiti juu ya virusi vya corona

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Taasisi ya Pasteur nchini Senegal inafanya utafiti juu ya virusi vya corona

Kufikia sasa ahead hiyo imetimizwa na mataifa matano pekee kati ya mataifa 54 - hali ambayo inaathiri utafiti wa kisayansi

Afrika in a utajiri wa wataalamu, lakini wanasayansi wake wanaenda kufanya kazi kwingine kutokana na ukosefu wa uwekezaji katika kazi yao - hii inamaanisha utafiti kutoka Afrika unalemazwa na changamoto zinazokabili sekta ya afya na ambazo hazipewi ufumbuzi.

Wale wanaoamua kusalia nchi mwao wanapata ugumu kubuni ushirikiano, kwasababu wafadhili wanaamua kufanya kazi nchi ammbazo zina miundombinu nzuri ya afya ambayo ni ya kutegemewa, kumaanisha kuwa majaribio ya change mara nyingi hufanyiwa Misri na Afrika Kusini.