Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya Corona: Raia 246 wa Tanzania waliokwama India warejea nyumbani
Iliyochapishwa
Kwa kipindi chote cha hatua ya kusalia ndani nchini India, Bi Saada alikuwa anakaa chumbani tu akitoka ni kuchukua chakula na kurejea tena chumbani. Baada ya kuwasili Tanzania, serikali imewapima ugonjwa wa Covid-19 na kufanya vipimo vinginevyo kama joto la mwili. Na kipindi wanasubiri majibu, wanatakiwa kujiweka karantini nyumbani kwa wiki mbili ambako serikali itakuwa inawafuatilia.