Virusi vy corona: Tanzania yasema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi

Iliyochapishwa

Serikali ya Tanzania imekana madai kwamba taifa hilo linajikokota katika vita dhidi ya virusi vya corona

Akizungumza na BBC msemaji wa serikali Dkt. Hassan Abbas amesema kwamba maabara kuu ya serikali bado imefungwa na vipimo kusitishwa kutokana na uchunguzi unaofanyiwa vifaa vya kupima Covid-19, lakini ikaongezea kwamba wagonjwa wa corona wanaendelea kupata matibabu huku wale wenye dalili wakitakiwa kujitokeza katika vituo vya Afya ili kufanyiwa uchunguzi..