Virusi vya corona: Mhandisi India abuni pikipiki ya kipekee

Maelezo ya video, Virusi vya corona: Pikipiki unayomwezesha mwendeshaji 'kutokaribiana’ na abiria
Iliyochapishwa

Mhandisi mmoja nchini India amebuni piki piki inayomwezesha mwendeshaji kuweka umbali wa mita moja kati yake na abiria wake katika juhudi za kukabiliana na janga la corona. Alitaka kutoa twaswira ya usafiri wa pikipiki baada ya mlipuko wa virusi vya corona. Pikipiki hiyo iliyoundwa kwa ubunifu wa hali ya juu inamwezesha abiria kushikilia usukani wake.