Virusi vya corona: Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga amesema Rais Magufuli ''anashauriwa vibaya''

Iliyochapishwa

Akijibu kauli za Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, Mbunge wa Tanzania kutoka chama tawala cha CCM Job Lusinde Kibabaje amesema mfumo ambao Magufuli anautumia katika kukabiliana na Covid -19 ni mfumo umewasaidia sana Watanzania tofauti na Afrika Kusini, Uganda Kenya na Rwanda. ‘’Pengine wanashindwa tu kumuelewa’’, alisema katika mahojiano na BBC.

‘’Rais mfumo alioutumia kwa kukataa kuwaweka watu Lockdown, sisi Watanzania tunafahamiana, kuna watu wengi wanakula chakula cha leo wakitoka...leo ukiwafungia ndani wanaweza kupata matatizo makubwa’’ amesema .

‘’Mi natakaka tu kumuambia mwanasiasa mkongwe Raila kuwa Magufuli anawafahamu Watanzania zaidi na rais ana uchungu zaidi na Watanzania kuhusu uchungu wowote’’alisema Mbunge Kibabaja.

Raila amesema viongozi wa kanda wamekua wakitaka kushauriana na rais John Pombe Magufuli, bila mafanikio.

Video: SABC