Virusi vya corona: Changamoto ya kuosha mikono wakati kuna uhaba wa maji

Maelezo ya video, Unawezaje kunawa mikono licha ya upungufu wa maji?
Iliyochapishwa

Kunawa mikono ni njia moja ya kukabiliana na virusi vya corona lakini kwa mataifa mengi ya Afrika kuna uhaba wa maji. Sasa je unawezaje kuhakikisha uko salama wakati maji yenyewe kupatikana ni changamoto? Guy Mbayo kutoka Shirika la Afya Duniani anatoa mawazo yake.