Coronavirus: Athari za kiuchumi zaanza kuonekana
Iliyochapishwa
Kenya ni miongoni mwa mataifa 26 barani Afrika ambayo yametangaza kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Kufikia sasa, watu wanne wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo huku wengine wakifanyiwa uchunguzi kubaini ikiwa wameambukizwa virusi hivyo.
Jijini Nairobi biashara imeathiriwa huku wengi wakihofia afya zao.