Trump afichwa maeneo ya aibu India

Maelezo ya video, Trump afichwa maeneo ya aibu India
Iliyochapishwa

Ziara ya Trump inatarajiwa kufanyika jimboni Gujarat, yalipo makazi ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Macho yote yatakua mji mkuu Ahmedabad, ambako Trump anasema anatarajia mamilioni ya watu kumkaribisha.

Lakini wakazi wa maeneo duni hawajali kuhusu ziara hii, wakiwemo wale waliofichwa nyuma ya ukuta na wale baadhi waliopata notisi ya kuyahama makazi yao.