BBC Africa Eye: imegundua vitendo vya mateso vinavyotekelezwa na polisi

Maelezo ya video, BBC Africa Eye: imegundua vitendo vya mateso vinavyotekelezwa na polisi
Iliyochapishwa

Utesaji ni kinyume cha sheria nchini Nigeria. Lakini picha kutoka kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha kuwa aina fulani ya mateso- njia ijulikanayo kwa jina ‘tabay’ hutumika kwa kiasi kikubwa wakati wa mahojiano na wakati wa kuwaadhibu wanaowashikilia, wakiwemo watoto.

Uchunguzi huu unatazama asili ya mbinu hii, umewabaini watu wanaofanya vitendo hivi, na kuhoji kwa nini hawawajibishwi.

Uchunguzi umebaini kuwa mnamo mwaka 2014, afisa mkuu wa polisi alihusika na vitendo hivyo vya utesaji dhidi ya kijana mmoja ambaye baadae alipoteza maisha kutokana na majeraha.