Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Muziki watumika kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa akili
Iliyochapishwa
Asilimia moja ya watu duniani wanazaliwa wakiwa na matatizo ya akili na ubongo, hali ambayo huwa inawafanya maisha yao kuwa magumu.
Huko Visiwani Zanzibar, chuo cha muziki kimeanzisha darasa maalum kwa watoto wenye utindio wa ubongo na matatizo ya akili kwa ujumla.
Mbinu hiyo ya kutumia muziki inasaidia kuwawezesha kuanza kuwa na ueleo wa kuwasiliana na kuzungumza na kujifunza kufanya shughuli mbalimbali wenyewe katika jamii.