Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Sikuwahi kuona picha ya mtu mlemavu mtandaoni'
Iliyochapishwa
Hannah alikatwa mikono yote na miguu miaka miwili iliyopita ili kuokoa maisha yake baada ya kupatwa na ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo. Alipokuwa anakuwa hakuwahi kuona picha ya mtu aliyekatwa kiungo cha mwili kwama yeye ikiwekwa mtandaoni na alitaka kujaza pengo hilo. Amekuwa akiangazia safari ya maisha yake katika mitandao ya kijamii na kutumia simulizi zake kuwapa motisha wengine wanaopitia hali ngumu maishani ili wasikate tamaa.