Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais Trump amewasilisha mpango wa amani wa Mashariki ya kati
Iliyochapishwa
Rais Trump amewasilisha mpango wa amani wa Mashariki ya kati na kuonya kwamba huenda ikawa ni fursa ya mwisho kwa Palestina kujipatia uhuru wake.
Chini ya mapendekezo yake, Jerusalem itasalia kuwa mji mkuu bila kutengwa na Israel, pamoja na kuhakikishia usalama wake.
Bwana Trump amesema mpango wake utasaidia kuundwa kwa mpaka wa pamoja na Palestina na kupata usaidizi wa kifedha iwapo watatimiza makubaliano yatakayofikiwa.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametupilia mbali mipango iliyopendekezwa na kusema hiyo ni njama tu.