Mwanamke anayetumia mieleka kuwakabili wabakaji DRC

Iliyochapishwa

Katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mieleka imemsaidia mwanamke mmoja kujikinga dhidi ya wabakaji katika barabara za mji huo alikokulia kama mpiganaji,

Shaki amewavutia watoto wengi wa kurandaranda mitaani na nyumbani kwake kumekuwa kimbilio kwa wasichana wanaojaribu kijikinga dhidi ya majambazi, wabakaji na magawadi wa mitaa ya mabanda ya Kinshasa.

BBC Afrika Eye imemfuatlia Shaki akijaribu kujifunza mieleka na kupigana ili aweze kumtunza binti yake na kuwapa mafunzo wanawake wengine wenye mtazamo tofauti jinsi ya kuwatunza wasichana