Watu 22 wauwawa na wengine zaidi ya 1000 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi

People stand outside collapsed building - 24 January

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Tetemeko la ardhi liliosababisha majengo mengi kuanguka
Iliyochapishwa

Watu wapatao 22 wameuwawa na wengine zaidi ya 1000 wamejeruhiwa na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mashariki mwa Uturuki.

Tetemeko lenye ukubwa wa richa 6.8 limepiga katikati ya mji wa Sivrice katika jimbo la Elazig na kusababisha majengo kuanguka na watu kufa na wengine kujeruhiwa huku wengine wakibaki bila makazi.

Watu 39 wameweza kuondolewa katika maeneo ambayo yaliharibiwa vibaya na wengine 20 wanahofiwa kuwa bado wamekwama ndani, waokoaji walisema.

Matetemeko ya ardhi huwa yanatokea mara kwa mara Uturuki, watu takribani 17,000 walifariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea magharibi mwa mji wa Izmit mwaka1999 lenye uzani wa zaidi ya 7 katika kipimo cha rikta .

Uturuki hukabiliwa na matetemeko ya ardhi kwa sababu nchi hiyo iko kwenye miamba ya kijiolojia yenye ufa.

Tetemeko la usiku wa ijumaa kuamkia jumamisi majira ya usiku, liliweza kufika katika nchi jirani za Syria, Lebanon na Iran.

A woman is pulled from the rubble in Elazig, Turkey. Photo: 25 January 2020

Chanzo cha picha, EPA

Watu zaidi ya 200 waliripotiwa kupata athari ya hapo hapo.

Mamlaka ya Uturuki, kitengo cha dharura kimesema kuwa tayari kimetuma kikosi cha uokozi cha watu zaidi ya 400 katika ukanda huo, wakiwa pamoja na turubahi na magodoro kwa wale waliopoteza makazi.

Imetangazwa kuwa watu wasirejee katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko hilo.

Gavana awali aisema kuwa ni watu sita tu ndio wamefariki katika tukio hilo.

Wengine waiookolewa walifariki hospitalini baada ya muda mfupi.

Mji ambao ulipata tetemeko hilo la ardhi , ni takribani kilomita 550 kutoka mji mkuu wa Ankara,ni mbali kidogo ya mji na kuna idadi kubwa ya watu hivyo ilikuwa kazi kwa huduma ya dharura kuwafikia kwa wakati.

Map: Turkey

Maofisa wanasema kuwa tayari wamepeleka mashuka, blanketi na turubahi katika eneo hilo.

Mamlaka imesema kuwa nyuzi joto imeshuka kwa sentigredi 8.

Chama cha msalaba mwekundu, Uturuki kimeweza kutoa msaada kwa mamia ya watu waliopata janga hilo.

Mji huo wenye watu wapatao 4,000 people, ni maarufu kwa watalii wanaokuja kuona fukwe za ziwa Hazar na chanzo cha mto Tigris.

line