Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamke aliyeugua saratani apata sura mpya
Iliyochapishwa
Denise Vicentin alipoteza jicho moja na sehemu ya taya yake baada ya kuugua saratani na kupata uvimbe mkubwa usoni miaka 30 iliyopita. Bi Denise ameweza kupata sura mpya na kurejea katika maisha yake ya kawaida. Watafiti katika chuo kikuu cha Paulista mjini Sao Paulo wametumia njia ya gharama ya chini kutengeneza sehemu ya uso wake. Wanadai walitumia simu ya teknolojia ya kisasa na kompyuta tu.