Je umawahi kuiona ndizi ghali zaidi duniani?

Maelezo ya video, Je umawahi kuiona ndizi ghali zaidi duniani?
Iliyochapishwa

Msaani mzaliwa wa eneo la Georgia Marekani, David Datuna amekula ndizi iliyotumika katika kazi ya sanaa ya Maurizo Cattelan ambayo iliuzwa kwa kitita cha dola $120,000.

Sanaa hiyo kwa jina 'Comedian' ilikuwa katika maonyesho ya Sanaa ya Basel mjini Miami Marekani, ambayo ndio sehemu yenye maonyesho ya sanaa zenye hadhi ya juu duniani.

Imewekwa ndizi nyengine hivyo basi hakuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya Datuna – ambaye alisema kwamba hatua ya kula ndizi hiyo inaharibu ‘maonyesho ya sanaa’.