Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi mvua kubwa zinavyohatirisha usalama wa watu na mali Afrika Mashariki
Iliyochapishwa
Mafuriko makubwa yameathiri maeneo mengi ya nchi za Afrika Mashariki zikiwemo; Somalia, Kenya, Sudan Kusini, Ethiopia na hata Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya mvua kubwa iliyonyesha kwa kipindi cha miezi miwili.
Umoja wa Mataifa (UN) umesema kuwa mamia ya watu wamekufa na maelfu kukosa makazi.