Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waziri wa maswala ya Kigeni Tanzania Paramagamba Kabudi awaomba Wakenya kuiga mfano wa Watanzania
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Paramagamba Kabudi aliwachemsha viongozi wa Kenya wakati wa uzinduzi wa ripoti ya BBI nchini Kenya akisema kwamba wanafaa kuwaiga wenzao wa Tanzania kwa kupinga ukabila.
Kabudi amesema kwamba ijapokuwa Kenya ni taifa kubwa lenye watu wazuri ukabila umekuwa ukiwarudisha nyuma.
Amewataka raia wa taifa hilo kuwa na Umoja na kufanya siasa za mshikamo na maendeleo badala ya siasa za kupigania mamlaka.
Aliwapongeza rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kwa kumaliza uhasama wao wa kisiasa baada ya uchaguzi wa 2017.