Maandamano dhidi ya mauaji ya maafisa wa Ebola huko Ituri yafanyika DRC
Wanaharakati kutoka kundi moja la kupigania haki za kibinadamu LUCHA (Lutte Pour Le Changement, or 'struggle for change'), na wale wa Oparesheni Filimbi (Whistle Blowers) wamekongamana katika mji wa Goma katika afisi ya ujumbe wa Umoja wa mataifa UN nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kupinga mauaji dhidi ya wafanyakazi watatu wa Ebola ambao ni wenyeji.
Shambulio hilo katika vituo viwili vya matibabu lililofanyika katika eneo la Ituri linadaiwa kutekelezwa na waasi wa Maimai ambao ni wapiganaji kutoka eneo hilo.
Wanaharakati hao pia wamekasirishwa na mauaji ya wanakijiji 19 katika kijiji cha Maleki, mjini Beni karibu na mpaka na Uganda.
Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na waasi wa ADF.
Waandamanaji sasa wanashinikiza walinda usalama wa Umoja wa mataifa nchini DRC waondoke.
Video na Byobe Malenga.