China yapinga kuwepo kwa 'jela' ya Waislamu nchini humo
Iliyochapishwa
Stakhabadhi zilizofichuliwa zinaonyesha kwa mara ya kwanza maelezo ya jinsi China inavyowateka akili mamia ya maelfu ya Waislamu katika jela moja
Serikali ya China mara kwa mara imesisitiza kwamba kambi hiyo iliopo magharibi mwa jimbo la Xinjiang inatoa elimu ya kujitolea na mafunzo.
Lakini stakhabadhi rasmi zilizoonekana na kipindi cha BBC Panorama, zinaonyesha jinsi wafungwa wanazuiliwa kutekwa akili na kuadhibiwa.
Balozi wa China nchini Uingereza Liu Xiaoming alifutilia mbali madai hayo akisema kuwa stakhabadhi hizo ni feki.
Alisema kwamba hatua hiyo imewalinda raia wa taifa hilo na kwamba hakuna hata shambulio moja la kigaidi katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.