Nelson Asani: Mashuhuda asimuilia ajali ya ndege DRC ilivyofanyika

Maelezo ya sauti, Nelson Asani: Alishuhudia ajali ya ndege DRC
Iliyochapishwa

Nelson Asumani ambaye alishuhudia ajali ya ndege iliyotokea siku ya Jumapili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimulia BBC alichokiona muda mfupi kabla ya ndege aina ya Doenier 228 kuanguka katka eneo la makaazi katika mji wa Goma mashariki mwa nchi hiyo na kuwaua abiria wote na rubani pamoja na watu waliokuwa katika nyumba hiyo.

Ndege hiyo ilianguka baada ya kushindwa kupaa katika uwanja wa ndege wa mji huo.