Cybertruck: Tesla yapata aibu wakati wa uzinduzi wa gari lake la umeme

Iliyochapishwa

Tesla imezindua gari linalotumia umeme ambalo hatahivyo liliiaibisha kampuni hiyo wakati wa uzinduzi huo.

Wakati walipokuwa wakionesha jinsi madirisha ya gari hilo yalioundwa na glasi isiyovunjika - kwa bahati mbaya wakati wa maonesho yalivunjika.

Elon Musk alisikika akitukana kabla ya kutoa mzaha kwa kusema: 'Kuna muda wa marekebisho'

Hatahivyo kampuni hiyo imepokea maagizo 150,000 ya kununua magari yake aina ya pickup kutoka kwa wateja wake , kulingana na Elon Musk licha ya aibu wakati wa uzinduzi wa magari hayo.