Tanzania imekasirishwa na hatua ya kuzuiliwa ndege yake Canada

Iliyochapishwa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amethibitisha kukamatwa kwa ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni.

Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini

Sababu ya kukamatwa kwa ndege hiyo, kwa mujibu wa Profesa Kabudi ni kesi iliyofunguliwa na mkulima mstaafu raia wa Namibia Hermanus Steyn.

Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.