Maryam Hamdani: 'Nilijifunza mwenyewe kupiga muziki wa taarab mtandaoni

Iliyochapishwa

Maryam Mohammed Hamdani anasema yeye ni mwanamke wa kwanza kupiga hadharani chombo cha muziki wa taarabu kijulikanacho kama Ganun.

Muziki huo wa taarabu asili yake ni Zanzibar na maeneo ya pwani za Afrika mashariki kwa ujumla.

Maryam anasema hakuweza kujifunza kupiga chombo hicho cha taarab akiwa mtoto kwa sababu ya masharti ya utamaduni, lakini sasa anasaidia kuwafundisha wanawake wengine kupiga muziki huo

BBC ilikutana nae...