Pakistan: Namna msichana mmoja alivyopambana kupata elimu

Chuo cha Sardar Bahadur mjini Quetta
Iliyochapishwa

Kwa miaka kadhaa, watu wenye silaha waliizunguka shule ya wasichana katika kijiji kimoja katika eneo la Balochistan nchini Pakistan, kuwazuia wasichana kuingia darasani, lakini hatimaye mmoja wa wasichana alifanikiwa kufika chuo kikuu na sasa anajiandaa kuwa mwandishi wa habari.Ameieleza BBC taabu alizozipitia.

''Kipindi changu chote cha utoto nimekuwa kwenye hofu,'' anasema Naeema Zehri, mwanafunzi katika chuo cha wanawake. ''Lakini bado inanipa hofu ninapofikiria niliyoyapitia.''

Naeema alikuwa katika kijiji kimoja kilichopo katika jimbo la Balochistan. Anasema wanaume wengi walikuwa wakitekwa na kuuawa katika mashambulizi ya makusudi.Hofu na silaha zilikuwepo kila mahali.

Balochistan ni eneo masikini nchini Pakistan, limeshuhudia mapigano ya muda mrefu kati ya wanamgambo na Jeshi la Pakistan.Katika vijiji vyake vilivyo milimani , maisha kwa ujumla yalikuwa mabaya sana, hasa kwa wanawake walipata shida sana,Naeema ameeleza.

''Utoto wangu ulitawaliwa na umasikini.Tuko watoto saba na Baba yetu alituacha na kuoa mwanamke mwingine. Mama yangu hakupata elimu, hivyo tulitegemea misaada kupata mahitaji yetu ya kila siku.Elimu ilikuwa anasa hatukuweza kugharamia.

Kwa Naeema, kupata elimu ilikuwa kwa mbinde. Alisoma kwenye shule ya wasichana ya serikali kwenye kijiji chake mpaka alipofika miaka 10, lakini shule ilifungwa.

Anasema kuwa kuanzia mwaka 2009 mpaka mwaka 2013 shule ilidhibitiwa na wahalifu na kuwekwa vizuizi kwenye eneo la kuingilia shuleni, kuwafanya wasichana wasiingie kwenye majengo ya shule.

''Walikuwa watu wenye silaha sita mpaka nane wakati wote.Ninakumbuka nilipokuwa nikipita eneo la shule nilipokuwa mtoto. tulikuwa tukitishwa na watu wenye silaha waliokuwa wamesimama nje ya shule.Nilikuwa nikihofu wanaweza kunifyatulia risasi.''

Chuo cha Sardar Bahadur Khan

Chanzo cha picha, Naeema Zehri

'Msipeleke watoto shuleni''

Watu wenye silaha walikuwa hawawatishi watoto, Naeema alisema, lakini kundi hilo lilikuwa na sababu mbili: kuwazuia wasichana wasipate elimu, ili watu wenye silaha waweze kutumia maeneo hayo ya shule kujificha.

''Ulikuwa ujumbe wa wazi kwa watu,'' msipeleke wasichana wenu shuleni.''alisema.

Madhara yaliyojitokeza kwenye kijiji yalikuwa ya kutisha. Walimu wa serikali hawakuthubutu kufanya kazi kwenye mazingira hayo, Naeema na wasichana wengine wachache walipelekwa kwenye shule nyingine kijiji cha karibu.

Wazazi waliwapeleka wasichana kwenye shule hiyo ili kupata mafuta ya kupikia ya bure yaliyokuwa yakitolewa bure na shirika la msaada la kimataifa ili kuongeza idadi ya wasichana kujiunga na masomo-lakini si kusoma.Kulikuwa na orodha ya wasichana walikuwa wakiitwa majina kisha kwenda nyumbani. Naeema anasema walimu walikuwa wakiogopa, lakini kiasi walikuwa wanapokea rushwa.

''Kulikuwa na shule nyingi zilizokuwa zinaonekana kwenye makaratasi pekee. Waalimu walipelekwa kwenye shule hizo na kuchukua mishahara pia-lakini shule zilikuwa hazifanyi kazi kabisa,'' alisema.

Wakati huo huo, machafuko jimboni Balochistan yalikuwa yakipamba moto. Ndugu wa wawili wa Naeema walitekwa nyara, miili yao ilipatikana miezi kadhaa baadae.

''Nilipatwa na bumbuwazi kabisa.Walikuwa wadogo sana, wenye ndoto za maisha; sikukisahau kifo chao kwa muda mrefu.''

Pamoja na hayo Naeema aliendelea na elimu yake.Baada ya kumaliza shule ya sekondari, alilazimika kusitisha kwenda shuleni lakini hakukata tamaa.

''Familia yangu haikuweza kumudu gharama za elimu, na pia walikuwa wanakabiliwa na changamoto kadhaa kutoka kwa wanakijiji.''

Hii ni kwa sababu wanawake hawakupewa msukumo wa kupata elimu, alisema -Isipokuwa tu elimu ya dini.

Wakazi wa Balochistan

Chanzo cha picha, Getty Images

Naeema aliendelea na masomo yake akiwa nyumbani, kama mtahiniwa binafsi. Alipomaliza elimu ya sekondari, elimu yake iliingiliwa na kaka zake waliokuwa wakiipinga. Lakini kuuawa kwa nduguze kulimpatia nguvu mpya. Alieleza kuwa kulikuwa kuna ukimya mkubwa kwenye vyombo vya habari.

Nikajiuliza watu wa Balochistan si binaadamu? kwa nini maisha yao si kitu? iliniuma sana,'' aliyoyapitia yalimfanya achukue masomo ya uandishi wa habari.

'Kusimulia simulizi kuhusu watu wangu''

Vyombo vya habari vya kimataifa haviruhusiwi kuripoti kutokea Balochistan isipokuwa kwa ruhusa kutoka kwa mamlaka-vibali ambavyo ni nadra kutolewa.

Naeema amesema kuwa aliposikia kuhusu chuo cha wanawake pekee , aliiambia familia yake wamuache aendelee na masomo.Kaka zake walikataa lakini mjomba wake mmoja alimuunga mkono na kumlipia karo kwa mwaka mmoja.Baada ya hapo hakuwa na fedha tena-lakini aliomba ufadhili wa USAID, fedha zinazotolewa na serikali ya Marekani,na sasa gharama za elimu zimelipwa. ''Na acha nikwambie,sitaogopa wakati wote nitasimamia ukweli.