Dr Marijuana Pepsi: Walinikejeli wakidai jina langu ni la ajabu

Dr Pepsi

Chanzo cha picha, Dr Marijuana Pepsi Vandyck

Iliyochapishwa

Mwanamke aliyekataa kubadili jina lake amewashinda watu waliokuwa wakimkejeli kwa kupata shahada yake ya uzamivu na kuwa dokta.

Marijuana Pepsi Vandyck amesema maisha yake yote jina lake limekuwa likionekana kichekesho kwa watu.

Lakini badala ya kubadilisha jina aliamua kujivunia jina lake.

Mwanamama huyo mwenye miaka 46 alitumia uzoefu wake katika kufanya utafiti kuhusu majina ya watu wenye asili ya weusi na namna gani yameathiri elimu ya watoto nchini Marekani.

Akikumbuka mazungumzo yake na mama yake alipokuwa mdogo kuhusu kwa nini alipewa jina la Marijuana Pepsi, alisema: Mama yangu aliniambia jina lako litakupeleka duniani kote.

Dr Pepsi na Mama yake

Chanzo cha picha, Marijuana Pepsi Vandyck

''Wakati wote nilifikiri, lakini nilijiambia kuwa mama yangu ni mwerevu, ana akili nyingi, nilimuamini.''

Marijuna alikuwa na miaka tisa kwa mara ya kwanza alipogundua kuwa ana jina lisilo la kawaida. Shuleni huko Wisconsin alisema si watoto tu waliokuwa wakilizungumzia jina lake bali pia waalimu. ''Waambie jina lako mpendwa,'' walikuwa wakimwambia.

''Marijuana si jina la kawaida kisha uongeze jina Pepsi na namna watu walivyokuwa wakiliongelea hawakuacha na mpaka sasa hawajaacha'' aliiambia BBC

''Waliniomba waniite Mary, na mara ya kwanza ilikuwa sawa, mpaka pale niliposhinda mashindano ya herufi.Nilirudi nyumbani na cheti, na mama yangu alikasirika sana alipoona cheti kinasomeka jina la Mary Jackson.

''Aliniambia nisiruhusu waniite Mary tena kisha aliekea shuleni na kuwataka wabadili jina.Hakuwa akitania.''

Lakini alipofika sekondari maswali kuhusu jina lake lisilo la kawaida na namna walivyokuwa wakiliongelea viligeuka kuwa maumivu. ''Nilipokuwa darasa la nne ilikuwa ajabu lakini sekondari ikawa kejeli.

''Ikawa kama silaha kwao, nilivumilia mengi. Siku moja nikaamua kuwa imetosha, siwezi kuvumilia zaidi,''

Marijuana anasema familia yake ilimsaidia kumpa nguvu ya kukabiliana na maneno mabaya na kubadili tabia yake.

Mwezi uliopita alipata shahada yake ya uzamivu katika masuala ya utawala wa elimu ya juu ya chuo kikuu cha Cardinal Stritch baada ya utafiti wake, kwa jina :''Majina ya watu wa asili ya weusi kwenye madarasa ya watu weupe-tabia za waalimu na mitazamo ya wanafunzo''.

Dr Pepsi

Chanzo cha picha, Marijuana Pepsi Vandyck

''Ingawa nilikuwa na tatizo na jina langu, sikufikiria sana namna litakavyoweza kuwaathiri wengine''.Alisema.

Siku ya kwanza ya muhula nikifanya kazi ya ualimu, alikumbuka mfanya kazi mwenzie akilalamika kwa mkuu wa chuo kuhusu orodha ya wanafunzi atakaowafundisha mwaka huo.

''Ninawauliza wengine kimetokea nini wakaniambia, 'Marijuana tazama majina, ni majina, alihukumu kutokana na majina ya watoto wenye asili ya weusi, nikafikiria kuwa huu ni ujinga, Nitaandika kuhusu jambo hili.''

Ameolewa na anaishi na mumewe na mtoto wake katika jimbo la Illinois, akifanya kazi ya kuwasaidia wanafunzi wa chuoni.

''Sisi ni binaadamu, lakini tunakosea tunaposikia majina kwa mara ya kwanza na kuanza kutoa maoni na kuhukumu.