Kwanini ni 'marufuku' kula mchana wa mwezi wa Ramadhan visiwani Zanzibar
Iliyochapishwa
Tendo kubwa ambalo linaonekana moja kwa moja kufanywa na waislamu katika kipindi hiki cha mfungo ni kujizuia kunywa na kula kutoka alfajiri (kuchomoza kwa jua) mpaka magharibi (kuzama kwa jua).
Visiwani Zanzibar, kula hadharani wakati wa mchana wa Ramadhan ni jambo ambalo hupigwa marufuku na mamlaka.
Japo visiwa vivyo havifuati sheria za kiislamu, wengi wa wakaazi wake ni waislamu na dini hiyo inaathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya kijamii visiwani humo.
Katika mazingira hayo, migahawa ya chakula hufungwa wakati wote wa mchana na kufunguliwa mara tu baada ya muadhini wa sala ya magharibi.
Je watu ambao hawafungi wanapata vipi chakula cha mchana? Mwandishi wa BBC Eagan Salla alitembelea visiwa hivyo na hii ni taarifa yake.