''Tuliongea naye kwenye simu akasema MV Nyerere inakaribia kuondoka”

Iliyochapishwa

Salome Lusatu ni miongoni mwa wale walipoteza ndugu na jamaa zao katika mkasa wa kusikitisha wa kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere alasiri ya tarehe 20.09.2018, Mkasa uligrarimu Maisha ya watu 226

Kivuko vha Mv Nyerere kilikuwa kwenye safari zake za kawaida kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara kilipo pinduka na kuzama dakika chache kabla ya kukita nanga katika ufukwe wa Bwisya kisiwani Ukara

Salome tangu kumpoteza mumwe anasema Maisha yamekuwa ya upweke na anahofu mambo mengi yatabadilika kwani Mumewe walikuwa wakisaidia katika mambo mengi hayupo tena

Mwezi mmoja tangu kutokea kwa mkasa huo bado simanzi na majonzi zimeendelea kutawala katika kisiwa cha ukerewe

Mwandishi wa BBC Eagan Salla alimtembela mjane huyu.

Mtayarishaji: Eagan Salla.