Mwanamziki wa Rap kutoka Marekani Lil Wayne asamehewa na Donald Trump

Maelezo ya sauti, Mwanamziki wa Rap kutoka Marekani Lil Wayne asamehewa na Donald Trump
Iliyochapishwa

Nyota wa rap Lil Wayne na Kodak Black walikuwa kwenye orodha ya watu zaidi ya 140 ambao walipewa msamaha au walipunguziwa adhabu na Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Donald Trump siku yake ya mwisho kazini. Wayne aliyetamba kwa vibao kama hiki alipatikana akiwa amebeba bunduki na risasi huko Miami Desemba 2019. Lil Wayne alikabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10.