Drake ataka tuzo za muziki za Grammys zifutiliwe mbali
Iliyochapishwa
Drake ametaka Grammys kubadilishwa na badala yake kuwepo onyesho mpya la tuzo, baada ya wasanii kadhaa kutoteuliwa mwaka huu. Drake alikuwa akizungumza baada ya The Weeknd kutoteuliwa licha ya albamu yake ya After Hours kuwa ndio rekodi inayouzwa zaidi nchini Marekani, Grammys bado hawajajibu.
