Ahukumiwa miaka 11 gerezani kwa kumuua soko wa milimani

Iliyochapishwa

Mahakama nchini Uganda imemhukumu mtu mmoja miaka kumi na moja gerezani, kwa mauaji ya Sokwe mmoja wa milimani aliyefarki mwezi juni . Sokwe huyo aliejulikana kwa jina Rafiki - alikuwa ndio mzee na kiongozi wa kikundi cha zamani zaidi cha Sokwe wa milimani aliyewahi kuishi nchini humo . Alipatikana amekufa mapema Juni, kwa majeraha ya tumbo.