Lewis Hamilton amesema kuwa hana nia yoyote ya 'kuihama' Mercedes.
Iliyochapishwa
Dereva wa magari yaendayo kasi Lewis Hamilton anasema kwa sasa hafikirii kuhama kwenye timu yake ya Mercedes. Bingwa huyo wa Dunia ni mmoja wa madereva wenye uwezo mkubwa ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu wa mwaka huu wa 2020 licha ya changamoto ya virusi vya corona.
