Wachezaji wa Barcelona wapunguziwa mishahara
Iliyochapishwa
Ni wazi sasa kuwa wachezaji wa Barcelona watapunguziwa mishahara kwa asilimia 70 wakati huu wa janga la corona ili kuchangia kwa mishahara ya wafanyikazi wengine wasio wachezaji, kupata asilimia 100 ya mishahara yao. Lionel Messi amesema uamuzi huo ulichelewa kwa sababu walikuwa wanatafuta njia mwafaka ya kusaidia klabu hiyo.
