Muigizaji maarufu wa filamu Idris Elba atangaza kuambukizwa virusi vya Korona.
Iliyochapishwa
Kupitia mitandao ya kijamii- muigizaji maarufu raia wa Uingereza Idris Elba ametangaza kuwa ameambukizwa virusi vya Korona. Elba amesema kuwa licha ya kutokuwa na dalili zozote za ugonjwa huo- alipatana na mtu aliyeambukizwa na hivyo akaamua kufanyiwa vipimo. Amewasihi mashabiki wake kuchukua tahadhari ya kujilinda kutokana na maambukizi hayo.