Bilionea wa Kijapani amtafuta mwanamke atakayeandamana naye mwezini

Maelezo ya sauti, Bilionea wa Kijapani amtafuta mwanamke atakaye andamana naye mwezini
Iliyochapishwa

Bilionea wa Kijapan, Yusaku Maezawa anamtafuta mpenzi ambaye ataandamana naye katika safari yake ya kuelekea mwezini mwaka 2023. Bilionare huyo atakuwa abiria wa kwanza kusafiri mwezini. Hivi majuzi mahusiano na mchumba wake wa zamani Ayame Goriki yalitumbukia nyongo. Hivi sasa wanawake tofauti ulimwenguni wanatuma maombi kwa bilionea huyo kupitia mtandao wake.