Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mapenzi yamtumbukia nyongo mkurungezi mkuu wa McDonald's
Iliyochapishwa
Kampuni maarufu ya McDonald's imemfuta kazi Mkurugenzi Mkuu Mtendaji Steve Easterbrook, baada ya kubainika alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo. McDonald's ambayo ni kampuni ya Marekani inayojulikana zaidi kwa baga na vibanzi imesema mahusiano hayo yaliridhiwa na wawili hao lakini Bw. Easterbrook alikikuka kanuni za kampuni hiyo. Sema nzi kufia kidondani!
Je, ni makosa kuwa na mahusiano ya kimapenzi kazini?
Tujadiliane kwenye Facebook BBCSwahili